Hii haijawahi kutokea. Momo Telecommunications inazindua MobiThon — hackathon ya kila mwaka inayolenga kuhamasisha ubunifu, teknolojia na utatuzi wa changamoto halisi za Kitanzania.
Na hii si kwa developers pekee.
MobiThon iko wazi kwa watu binafsi, developers, startups, biashara na kampuni — yeyote mwenye idea au solution anayotaka kuijenga kwa kutumia Momo Business.
Zawadi
| Tuzo | Zawadi |
|---|---|
| Startup Bora | TZS 3,000,000 |
| Nafasi ya kwanza | TZS 2,500,000 |
| Nafasi ya pili | TZS 1,000,000 |
| Nafasi ya tatu | TZS 500,000 |
Nafasi tatu za juu ziko wazi kwa watu binafsi, startups, biashara na kampuni kwa usawa. Hupimwi kwa kipimo tofauti kwa sababu ya wewe ni nani.
Fainali
Kila anayefika fainali anawasilisha ana kwa ana Millennium Tower, Dar es Salaam — siku ile ile ambayo platform ya Momo Business inazinduliwa rasmi. Developers, waanzilishi, kampuni na waandishi wa habari wote wapo ukumbini.
Na hii si ya mwaka huu tu. MobiThon itafanyika kila mwaka, ikiwa jukwaa la kuwaunganisha developers, wajasiriamali, startups na wapenzi wa teknolojia, na kuhamasisha kizazi kipya cha solutions zilizojengwa Tanzania.
Jinsi ya kujiandikisha
Usajili unafanyika ndani ya akaunti yako ya Momo Business. Kama huna, kuifungua ni bure na inachukua dakika moja.
👉 Jiandikishe MobiThon · Soma masharti yote na maswali
Startups, kampuni na wadhamini
MobiThon si hackathon tu. Kila mwaka startups na technology companies tano — zenye bidhaa zisizoshindana na Momo Business — hupata nafasi ya kuonyesha bidhaa zao kwenye tukio, mbele ya developers, wabunifu na jamii ya teknolojia Tanzania.
Nafasi za udhamini pia zipo wazi: logo yako kwenye tukio, fursa ya kuzungumza, kampuni yako kuonyeshwa kwenye screen kubwa ya tukio, na uonekanaji zaidi wa brand yako.
👉 Omba nafasi ya kuonyesha au uulize kuhusu udhamini
MobiThon — Jenga. Buni. Shinda.